WAETHIOPIA WAANDAMANA KUPINGA SHERIA YA UGAIDI

Ethiopians hold an anti-government protest in Addis Ababa, June 3, 2013.


WAETHIOPIA wamemiminika katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa, kupinga sheria dhidi ya ugaidi.

Katika maandamano hayo yaliyoandaliwa na vyama vya upinzani, waandamanaji hao wanataka mageuzi ya kisiasa, usawa na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.


Kiongozi wa chama cha upinzani cha Unity for Democratic Justice (UDJ), Negasso Gidada, aliitaka serikali kuifuta sheria hiyo “kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa mara moja.”

naye mbunge wa upinzani, Girma Seifu alisema kuwa lengo la sheria ya ugaidi iliyowekwa mwaka 2009, ni kuzibana shughuli za taasisi za kiraia, shughuli za vyombo vya habari na zile vya vyama vya kisiasa.”


waandamanaji wanasema tokea sheria hiyo ilipowekwa serikali imekuwa ikiwaziba midomo Waethiopia wanatoa maoni yao dhidi ya sera za serikali. Hivyo, wanaitaka serikali ya Addis Ababa itoe tafsiri maalumu ya ugaidi.


Hata hivyo, serikali inasema kuwa upinzani unataka kuwatakasa magaidi waliotiwa hatiani na “wanacheza na hatari” inayoikabili Ethiopia kutokana na ugaidi.


kwa mujibu wa Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari yenye makao yake mjini New York Marekani, zaidi ya waandishi wa habari kumi wameshitakiwa chini ya sheria ya ugaidi. Kamati hiyo inasema kuwa Ethiopia ina idadi kubwa kabisa duniani ya waandishi wa habari waliokimbilia uhamishoni.


makundi ya haki za binadamu yanaituhumu serikali ya Ethiopia kwa kutumia sheria hiyo kuwakandamiza raia. Hata hivyo, katiba ya Ethiopia inatoa uhuru wa kujieleza kwa wananchi.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment