Katika hotuba yake jana mbele ya Hadhara kuu ya Umoja wa
Mataifa, Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, aliwashambulia mashoga na wasagaji na
kusema kuwa vitendo hivyo ni miongoni mwa “vitisho vikubwa kabisa kwa uwepo na
uhai wa jamii ya binadamu.”
Rais Jammeh alisema kuwa ushoga, tamaa na ubabe “ni
majanga makubwa kabisa kuliko majanga yote ya kiasili yakiwekwa pamoja.”
Maneno haya ya Rais Jammeh ni muendelezo wa msimamo wake
dhidi ya vitendo vya ushoga na usagaji. Mwaka 2008, aliwaambia mashoga na
wasagaji kuondoka nchini mwake la sivyo wakatwe vichwa.
Vilevile amekuwa akiandamwa na ukosoaji wa kimataifa kwa
kusema kuwa anaweza kutibu UKIMWI kwa dawa yake ya asili na ya mitishamba.
Rais Yahya Jammeh aliingia madarakani katika nchi hiyo
ya Afrika Magharibi mwaka 1994 kwa njia ya mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment