Umbali wa mita kadhaa kutoka ufukwe wa Pakistan
limetokea jambo la ajabu jana Jumanne tarehe 24 Septemba baada ya tetemeko
kubwa la ardhi lililoupiga mji wa Aoran katika jimbo la Balochistan lililo
kusini magharibi mwa Pakistan na kuua watu wasiopungua 328.
Ghafla kilionekana kisiwa mkabala na mji wa Gawadar
kusini magharibi mwa nchi hiyo. Kisiwa hicho kina takriban urefu wa mita 200,
upana ni mita 100 huku urefu wa kwenda juu ukiwa ni mita 20. Hayo ni kwa mujibu
wa Dk Asef Inam kutoka chuo cha taifa cha sayansi za bahari.
Lakini suala hilo limeibua swali: Je, kisiwa hicho
kimetokana na tetemeko hilo? Wataalamu wanatilia shaka suala hilo wakisisitiza
kuwa “tetemeko lilitokea mbali na mji wa Gawadar na kwamba matetemeko kama hayo
hayawezi kuleta matokeo ya aina hiyo.” Kwa mujibu wa mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha
Oregon Chris Gould Wenger, tetemeko la Tsunami ndilo linaloweza kusababisha
matokeo kama hayo ya kutokezea kwa kisiwa.
Hivyo basi, suala hilo linabaki kuwa lenye utata. Isipokuwa
baadhi ya waandishi wa habari wanadai kuwa kisiwa husika kiliibuka miaka 45
iliyopita kikapotea mwaka mmoja baada ya kuibukuka kwake.
CHANZO: France 24/ Arabic
PICHA MBALIMBALI ZA KISIWA HICHO
0 comments:
Post a Comment