MAAFISA wa Pakistan wanasema kuwa kwa uchache watu 327
wamethibitika kupoteza maisha na mamia kujeruhiwa baada ya tetemeko thakili la
ardhi kulipiga jimbo la kusini magharibi la Balochistan.
Zaidi ya watu 400 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo
lenye ukubwa wa 7.8 lililoitikisa miji kadhaa kama vile Karachi, Hyderabad,
Quetta na Kalat.
Ripoti za vyombo vya habari kutoka nchini humo zinasema
kuwa mifumo ya mawasiliano imeharibiwa vibaya sana katika maeneo hayo.
Maafisa wa hali ya hewa wanasema kuwa mitikisiko
ilisikika mpaka kwenye miji mingine kama mji mkuu wa India, New Delhi. Mitetemo
mingine midogo ilifuatia na kuutikisa ukanda wote wa eneo hilo.
Jeshi la Pakistan limelazimika kuingia kazini kufanya
shughuli za uokozi na kuwasambaza askari wapatao 200 katika eneo lote.
Jimbo la Balochistan ni eneo linalokumbwa na matetemeko
ya mara kwa mara. Tetemeko kama hilo liliua watu 41 mwezi Aprili.
0 comments:
Post a Comment