MAHAKAMA moja nchini China imemhukumu mtoto wa jenerali
mmoja wa nchi hiyo kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kubaka, baada ya kesi
yake kuvuta hisia za wananchi.
Li Tianyi, mwenye umri wa miaka 17, na wanaume wengine
wanne wamekutwa na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja katika hoteli moja mjini Beijing
mwezi Februari mwaka huu.
Baba yake anaitwa Li Shuangjiang, ni mwimbaji katika
jeshi na ana cheo cha jenerali katika jeshi la China.
Wakati wa kesi yake, vyombo vya habari viliripoti kuwa “hakukiri
kufanya hujuma ya kingono na hakukiri kuwa na uhusiano na mwanake husika, akisema
kuwa alikuwa amelewa na hakujua chochote” kilichotokea.
Washtakiwa wengine wanne katika kesi hiyo walihukumiwa
adhabu ya kifungo cha kati ya miaka 3 na 12.
Baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi kwamba Li asingehukumiwa
adhabu ya kifungo gerezani. Wengine walifurahishwa na hukumu hiyo iliyotolewa
jana alhamisi.
Baba yake ni mkuu wa idara ya sanaa katika chuo cha
jeshi la China, na ni maarufu kwa nyimbo za kizalendo. Mama yake, Meng Ge, naye
pi ni mwimbaji mkubwa.
CHANZO: Al-Jazeera
0 comments:
Post a Comment