NAIROBI, KENYA: Wakenya na ulimwengu mzima wanasubiri
kwa shauku kjua idadi kamili ya vifo vya shambulizi la Westgate baada ya
washambuliaji kudai kuwa waliua watu 137.
Familia zilipoteza watu wao wametishika sana huku
wataalamu wa kuchunguza mauaji wakichelewa kutoa miili ya wale waliokutwa na
mauti katika jengo hilo.
Mashirika ya habari ya BBC na Associated Press yaliandika
katika akaunti zao za twitter kwamba Al-Shabaab waliripoti kwamba waliwaua watu
137.
Vikosi vya usalama viliripoti kuwa sauti za mateka
zilisikika wakati wa dakika za mwisho za harakati za vikosi vya pamoja kulidhibiti
jengo hilo baada ya sehemu ya jengo hilo kuanguka.
Askari sita wa jeshi la Kenya ni miongoni mwa watu 69
waliouawa, kwa mujibu wa rekodi rasmi zilizotolewa na mamlaka za serikali. Askari
hao walihusika katika juhudi za kuwaokoa mateka waliokuwa wameshikiliwa na
watekaji.
Inaamini kuwa idadi ya mwisho itajulikana baada ya
wataalamu hao kuruhusu utoaji wa miili iliyofukiwa na kifusi ndani ya jengo
hilo. Mashuhuda waliofanikiwa kukimbilia
eneo salama walisema kuwa waliona miili kadhaa ya maiti ikiwa imelala sakafuni.
CHANZO: KTN Kenya
0 comments:
Post a Comment