WABUNGE WA IRAN WACHUKUA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YA RAIS AHMADINEJAD

President Mahmoud Ahmadinejad (L) accompanies Esfandiyar Rahim-Mashaei to the Interior Ministry on May 11, 2013.
Rais Mahmoud Ahmadinejad (kushoto) akimsindikiza Esfandiyar Rahim-Mashaei katika ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani Mei 11, 2013.




KUNDI la wabunge wa Iran wamechukua hatua ya kisheria dhidi ya Rais Mahmoud Ahmadinejad kwa kwenda kinyume na Sheria ya Uchaguzi baada ya kuonesha hadharani kuwa anamuunga mkono mshirika wake anayegombea urais.



Zaidi ya Wabunge 150 wamesaini waraka wa mashitaka dhidi ya Ahmadinejad kwa 'kitendo kinachokiuka sheria' cha kumsindikiza swahiba wake Esfandiyar Rahim-Mashaei kwenda kujiandikisha kwa ajili ya kuwania urais utakaofanyika Juni 14.


Wabunge hao wanasema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Iran inapiga marufuku matumizi ya rasilimali za umma kwa ajili ya kumpendelea au kutumika dhidi ya mgombea yeyote.


Rais Ahmadinejad amejitetea kwa kusema kuwa alikuwa na likizo siku ya Jumapili wakati walipomsindikiza Rahim-Mashaei kwenda wizara ya Mambo ya Ndani kwa ajili ya kujisajili. 

Baraza la Ulinzi wa Maslahi ya Kitaifa - chombo kikuu kinachosimamia uchaguzi - kimetangaza kuwa kitendo hicho cha Rais ni kinyume cha sheria.


Usajili wa wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa 11 urais nchini Iran ulifikia tamati siku ya Jumamosi huku wagombea wapatao 686 wakiwa wamejiandikisha kwa ajili ya kuwania kiti hicho.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment