FRANK RIBERY AKERWA MNO NA KITENDO CHA JEROME BOATENG CHA KUMMWAGIA POMBE

Ribery 'Bilal' akerwa mno  na kitendo cha Jerome Boateng cha kummwagia pombe





Frank Ribery mchezaji Muislamu wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa timu hiyo Jerome Boateng baada ya kumwagia mwilini  pombe, wakati wa wakishangilia ubingwa wa Bundesliga mwisho wa wiki iliyopita.

Mfaransa huyo ambaye ni mchamungu  wa swala tano  na ambaye jina lake la Kiislamu ni 'Bilal' alijaribu kumkimbia Boateng  ili aepukane  na kitendo cha ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo, ambapo Bayern Munich  walioshinda  3-0 dhidi ya Augsburg.

Lakini pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe ambayo ni haramu kwa mujibu wa dini yake,  Ribery hatimaye aliogeshwa na pombe hiyo mwili mzima na mchezaji mwenzake Boateng mwenye asili ya Kiafrika.

Ribery 'Bilal' alionyesha kukasirishwa mno na kitendo hicho, na kusisitiza kuwa:  'Sitaongea tena na Boateng, anajua mie ni Muislam. Nimechukizwa  sana na kitendo chake.'


Mlinzi David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk pia walijiunga na Boateng kumlowesha pombe  Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua kuwamwagia baadhi ya mashabiki walioonekana kupendezewa na ushangiliaji huo.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment