WAARABU WALIOKAMATWA ARUSHA WAACHIWA HURU



Habari zilizopatika zilizopatikana kutoka Dubai zinasema kuwa raia watatu wa Falme za Kiarabu waliokuwa wameshikiliwa nchini baada ya tukio la mlipuko wa bomu mjini Arusha wameachiwa huru na wamerudi kwako.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Khaleej daily, watu hao waliachiwa huru kwa msaada wa wizara ya mambo ya nje kufuatia "uratibu kati ya ubalozi wa Falme za Kiarabu na Tanzania."


Ripoti hiyo imevinukuu "vyanzo vya ndani" vikisema kuwa watatu hao wamesharejea nyumbani.



Siku ya Jumapili, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Saudi Arabia ilitangaza kuwa raia mmoja wa Kisaudi aliyekuwa wameshikiliwa pamoja na wenzake wa Falme za Kiarabu ameachiwa huru bila mashitaka yoyote baada ya kukutwa kuwa hawana hatia.



Msaudia huyo na raia watatu wa falme za Kiarabu alikamatwa pamoja na Watanzania watano baada ya mlipuko wa bomu uliotokea katika mjini Arusha, tukio lililoelezwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa ni "tukio la kigaidi."


Tukio hilo ni miongoni mwa matukio mabaya kabisa kuwa kulikumba taifa hili kwa miaka mingi.


Aidha, mbali na watu watatu waliokufa katika tukio hilo, watu wapatao 60 walijeruhiwa.


CHANZO: AFP
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment