WAASI WA PKK KUANZA KUONDOKA UTURUKI TAREHE 8 MEI

A file photo shows PKK fighters training at a base in northern Iraq.
Picha ya Maktaba ikiwaonesha waasi wa PKK wakifanya mazoezi katika ngome yao kaskazini mwa Iraq



Kundi la waasi wa PKK limesema kuwa wapiganaji wake wataanza kuondoka katika ardhi ya Uturuki mwenzi Mei kuelekea kaskazini mwa Iraq na kuhitimisha uasi wao dhidi ya Serikali ya Ankara uliodumu kwa miongo mitatu.


Shirika la habari la Firat linaloongozwa na kundi hilo lilimnukuu kamanda wa PKK Murat Karayilan akisema kuwa "Tutaanza kuandoka tarehe 8, Mei, 2013 kama sehemu ya utaratibu endelevu.



Karayilan alisema kuwa wataondoka kwa awamu na hatua hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo.


Aidha, alilitaka jeshi shupavu la Uturuki "kutofanya vitendo vyovyote vya kichokozi," akionya kuwa hilo likitokea, basi waasi hao watajibu mapigo na "uondokaji utasitishwa mara moja."


Inaaminika kuwa maelfu ya waasi wa PKK wanaishi katika milima nchini Uturuki, huku tawi la kijeshi la kundi hilo likiwa na makao makuu kaskazini mwa Iraq.


Mnamo Machi 21, kiongozi wa kundi hilo aliyeko gerezani Abdullah Ocalan aliwaamuru wapiganaji wake kuweka silaha chini na kuagiza usitishaji vita wa kihistoria kufuatia mazungumzo yake na maafisa wa Uturuki.


Serikali ya Uturuki ilianzisha mazungumzo na kiongozi huyo kwa lengo la kukomesha mgogoro huo uliodumu kwa muda wa miaka 30 ambao uligharimu maisha ya maelfu ya watu.


Kundi hilo lilianzisha mapigano mwaka 1984 dhidi ya Serikali ya Uturuki likitaka kujitenga kwa eneo la kusini mashariki linalokaliwa na watu wengi wa jamii ya Kikurdi.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment