HIZBULLAH YAKANUSHA VIKALI MADAI YA ISRAELI

An Israeli military naval ship and an Israeli air force helicopter operate next to a cruise ship off the coast of Haifa on April 25, 2013.
Meli na ndege ya jeshi la Israeli zikifanya operesheni nje kidogo ya pwani ya Haifa jana Aprili 25, 2013.





Harakati ya mapambano ya Hezbullah imekanusha vikali madai yaliyotolewa na maafisa wa jeshi la Israeli kwamba kundi hilo lilituma ndege isiyokuwa na rubani (drone) kwenye maeneo ya Palestina.


Kituo cha televisheni cha Al-Manar kiliweka tangazo la moja kwa moja lililokanusha madai hayo kwenye taarifa zake za jana Alhamisi.


Mapema siku hiyo, jeshi la Israeli lilidai kuwa limeiangusha 'drone' ya Hizbullah jirani na bandari ya kasikazini ya Haifa.



Msemaji wa jeshi alisema kuwa ndege hiyo ilitambuliwa ikiwa katika anga ya Lebanon kilometa nane (maili 5) kutoka pwani ya magharibi mwa Haifa na kudondoshwa na ndege ya jeshi la Israeli aina ya F-16.

Ndege iliyokuwa imembeba Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ambaye alikuwa akifanya ziara katika eneo la kaskazini la nchi hiyo, ililazimishwa kutua kufuatia hatua ya 'drone' hiyo kuingia katika anga la Israeli.

Katika taarifa yake, Netanyahu alisema kuwa tukio hilo ni “zito mno.” 

Inaelezwa kuwa meli za Israeli zinatafuta mahali ndege hiyo ilipodondokea.

Aidha, mwezi Oktoba, mwaka jana, ndege kama hiyo iliyotumwa na Hezbollah ilipenya ndani kabisa ya Israel kabla ya kuangushwa na makombora ya Israeli. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment