MISRI: WATU 8 WAUAWA NA 20 WAJERUHIWA KATIKA MAPIGANO BAINA YA WAKRISTO NA WAISLAMU

People inspect a destroyed room in a building which was burnt down during clashes between Christians and Muslims in al-Khusus town, Egypt, on April 6, 2013.
Watu wakitazama chumba kilichoharibiwa vibaya katika jengo lililochomwa moto wakati wa mapigano baina ya Wakristo na Wakristo katika mji wa al-Khusus, Misri, leo Aprili 6, 2013.




Kwa uchache watu 8 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya mapigano kuzuka baina ya Wakristo na Waislamu katika mji wa Al-Khusus jirani na mji mkuu wa Misri, Cairo.


Chanzo kimoja cha Usalama, kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kilisema kuwa Waristo 8 wa madhehebu ya Coptic na Muislamu mmoja waliuawa mapema Ijumaa baada ya wafuasi wa makundi hayo mawili kupambana katika mji wa al-Khusus, kilometa 12 (maili 7) kaskazini mashariki mwa Cairo.


Chanzo habari kimesema kuwa kundi la vijana wa Kikristo walikuwa wakichora msalaba kwenye ukuta wa Taasisi moja ya Kiislamu, na kusababisha mapambano baina ya wanafunzi wa taasisi hiyo na vijana wa Kikristo.

Vikosi vya Usalama vimeweza kudhibiti hali ya mambo na watu 15 wanashikiliwa kuhusiana na vurugu hizo.


Hii sio mara ya kwanza vurugu kutokea nchini humo baina ya Waislamu na Wakristo wa madhehebu ya Coptic ambapo huko nyuma mapigano kama hayo yameshagharimu maisha ya watu wengi.

Wakristo wa madhehebu ya Coptic ni asilimia 10 ya wananchi milioni 83 wa Misri.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment