LEBANON: WAZIRI MKUU MPYA APATIKANA

Lebanon
Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Tammam Salam




Tammam Salam ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Lebanon na kuahidi kuimarisha usalama dhidi ya mgogoro unaoendelea katika nchi jirani ya Syria.


Leo Rais wa nchi hiyo, Michel Sleiman alimtangaza rasmi, waziri wa zamani wa utamaduni, kuwa waziri mkuu na kumpa jukumu la kuunda serikali mpya.

  

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuteuliwa, Salam alisema kuwa ataitoa Lebabon  In his first speech after nomination, Salam said he would “bkatika hali ya sasa ya mgawanyiko na mgogoro wa kisiasa na kuiweka salama dhidi ya hali mbaya inayoendelea katika nchi jirani ya Syria.



Mgogoro wa Syria umevuka mpaka katika maeneo ya Lebanon, na mara kwa mara mapigano yamekywa yakiripotiwa kwenye maeneo ya mpakani.


Uteuzi wa Salam umekuja baada ya siku mbili za vikao vya bunge vilivyomalizika leo. Alipata kura 124 kutoka kwa wabunge 128.
 

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 67 amepata uungwaji mkono kutoka kwa makundi mawili hasimu katika siasa za Lebanon, mrengo wa Machi 14 na Machi 8.


Waziri Mkuu aliyemtanguliwa, Najib Mikati alijiuzulu mnamo Machi 22 baada ya msuguano katika baraza lake la mawaziri kuhusu maandalizi ya uchaguzi ujao wa bunge utakaofanyika mwezi Juni.


Mikati ataendelea kuongoza serikali mpaka waziri mkuu mpya, atakapounda serikali itakayoungwa mkono na mirengo hasimu ya kisiasa.



Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment