CANADA: WAWILI WAPIGWA RISASI KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO



Police officers holding a baby at the day care center in Gatineau, Quebec on April 5, 2013.



Shambulizi la risasi katika kituo kimoja cha kulelea watoto katika mji wa Quebec, nchini Canada, limegharimu maisha ya watu wasiopungua wawili akiwemo mfanyakazi mmoja.

Tukio hilo lilitokea jana Ijumaa katika kituo cha kulelea watoto cha Racines De Vie Montessori, kilichopo jirani na Mto Ottawa.

"Watu wawili wamekufa. Mmoja wao ni mtu aliyehusika na shambulizi na wa pili ni mfanyakazi katika kituo hiki," Mkuu wa Polisi wa Gatineau, Mario Harel alisema.

Maafisa wa kituo hicho wanasema kuwa watoto 53, ikiwa ni pamoja na watoto 5 wachanga, katika kituo hicho walihamishiwa eneo la jirani lenye salama wakati wa shambulizi hilo.

Polisi walieleza kuwa huwenda watoto hao wakawa wameshuhudia hayo mauaji.

Mkuu wa Polisi wa Gatineau, Mario Harel alisema kuwa mapema siku ya Ijumaa walipokea simu kuhusu mtu aliyekuwa na bunduki akiwatishia watu. Harel hakutoa maelezo zaidi juu ya utambulisho wa watu hao.

Alisema kuwa polisi wanafanya uchunguzi wa uhusiano kati ya watu hao wawili na kuangalia uwezekano wa tukio hilo kuwa na uhusiano na migogoro ya ndani.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment