'ziara ya obama msikiti wa al aqsa ni kutangaza vita'



Muonekano wa hekalu la mlimani Na ukuta wa maumivu,
katika mji wa zamani mashariki ya Al Quds

Wanamgambo wa hamas wameonya kwamba ziara ya rais wa marekani Balack Obama katika msikiti wa al aqsa uliopo mashariki ya palestina ni  kutangaza vita na waislamu dunia nzima.
 
Musheer al Masri, muwakilishi wa Hamas katika eneo la Msikiti wa al aqsa aliyasema maneno hayo wakati akiongea na kundi la wapalestina waliopo katika eneo lililo zingilwa la West Bank Juzi ijumaa.
Al Masri aliitisha mapambano ya tatu dhidi ya izrael, kama Obama atachagua kutembelea hekalu la mlimani, mahala ambapo msikiti wa al aqsa unapatikana.
Obama atatembea katika mipaka iliyovamiwa mapema mwezi huu, na tayari Washiongton imethibitisha ziara yake katika hekalu la mlimani.
Waziri mkuu wa palestina aliyechaguliwa kwa demokrasia, Ismail Haniyeh juzi ijumaa alieleza ziara hiyo ni kama mtego wa kushusha harakati za makubaliano zinazoendelea.
“tunashawishika kusema kuwa ziara ya Obama haitakuwa na faida yoyote kwa watu wetu” Alisema Ismail Haniyeh akihutubia ukanda wa gaza katika swala ya ijumaa.
Haniyeh pia alimueleza kiongozi wa mamlaka ya palestina, Mahmoud Abbas kwamba “asinase kwenye mtego wa ziara ya Obama katika eneo hilo na kufunga mlango wa makubaliano”
“ziara ya Obama italenga maendeleo ya eneo hili na sababu za mgogoro wetu katika hali ya kukandamiza wapalestina ili alete juhudi za kuanzisha upya upuuzi wanaouita makubaliano na izrael” haniye alisema.
Katika mkutano wake alhamis iliyopita  na viongozi wa jamii ya wayahudi waishio marekani iliyofanyika white house hakuashiria kama patakuwa na mazungumzo mapya na makubwa ya amani katika ziara yake mashariki ya kati.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment