Mwanamke wa ajabu, mguu wake una uzito wa kilo 107

Na Herieth Makweta
LANCASHIRE, Uingereza
JOPO la madaktari wamemwahidi mwanamke ambaye mguu wake unakua kila kukicha kuwa, wanamtafutia suluhu ya tatizo lake baada ya kupata ramani ya DNA yake.
Mandy Sellars, 38, hali yake kiafya imesababisha miguu yake kukua bila kukoma maisha yake yote.
Licha ya kuwa na tatizo hilo, Mandy alilazimika kukatwa mguu wake wa kushoto baada ya kuambukizwa virusi vya ‘septicaemia’.
Lakini baada ya miaka mitatu mguu wake huo ulianza kukua tena na mpaka sasa una uzito wa kilo 19.
Mandy hivi karibuni baada ya kupimwa maumbile yake hayo, madaktari hao waligundua kuwa ni binadamu wa kwanza kupatwa na maradhi hayo.
Hali hiyo inamsababisha, Mandy ashindwe kuzunguka na kusafiri sehemu mbalimbali, muda wote wa wiki hutumia akiwa nyumbani.
Akihitaji kusafiri hutumia kiti maalum kuweza kutembelea.
Madaktari walijaribu njia mbalimbali kuhakikisha kuwa wanasitisha hali hiyo, lakini mguu wake unaendelea kuongezeka, hadi sasa Mandy hana uwezo wa kutembea kutokana na uzito wa miguu yake.
“Mimi sioni kama kuna uwezekano wa kusimamisha hali hii,” alisema Mandy anayeishi huko Huncoat, Lancashire nchini Uingereza, Ninahitaji kubadili haya maisha nimeyachoka, natamani kuachiliwa kutoka hapa na nitoke nje mwenyewe nikaishi huko.”anasema.
Hali hiyo ya Mandy inaweza kupata uwezekano wa kupona baada ya wanasayansi kutoka, Chuo Kikuu cha Cambridge kuamua kuchukua nafasi ya kujaribu kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Mwaka jana Dk Robert Semple alichukua DNA ya Mandy kutoka katika sampuli ya tishu ya damu yake kwa ajili ya kupima tatizo alilonalo.
Hata ivyo utafiti huo ulibaini kuwa alikuwa na machafuko ya kipekee.
“Mimi ni mtu wa kwanza katika dunia kupatwa na tatizo hili ambalo mpaka sasa bado halijapatiwa jina,” alisema Mandy wakati akihojiwa na televisheni ya ITV kwenye kipindi cha This Morning.
“Nilipendekeza kwa Dk Semple kuwa ugonjwa huu auite Sellars Syndrome!” alisema Mandy huku akisisitiza kuwa katika majibu ya daktari Semple na timu yake walipendekeza apatiwe matibabu ya jeni.
Dk Semple anasema: “Nilianza kuchukua vipimo mwezi Septemba mwaka jana, na lengo lilikuwa ni kusitisha ukuaji wa miguu yake. Awali ya wote walianza kwa kuchukua vipimo vya DNA” alisema Semple.
Mandy anasema alikuwa amekata tamaa kutokana na hali yake, lakini utafiti wa Dk Semple ulimfanya mpaka sasa aweze kujua kuwa atapatiwa suluhu ya tatizo lake.
“Tatizo hili lilianza kuonekana toka nilivyozaliwa baada ya miguu yangu kuonekana ilikuwa ni mikubwa kuliko viungo vingine. Madaktari hawakujua haraka kwamba lilikuwa ni tatizo, hata hivyo walijidadisi sana. Hawakutaka mama yangu anione kwa wiki mbili. Hawakudhani kama nitaishi”anasema.
Mguu wake wa kushoto una urefu wa inchi tatu kuliko mguu wake wa kulia, na yote kwa pamoja ilikuwa na urefu usio sawa.  Lakini Mandy anasema alikua na alicheza na wenzake michezo mingi kama watoto wengine, ukiwemo mpira wa miguu.
Tatizo hilo lilianza kukua kwa kasi mwaka 2002 baada ya kupooza mgongo wake kwa miezi miwili, na wakati wote huo miguu yake ilikuwa ikiendelea kukua.Mwaka 2005 alipata maambukizi ya damu, kisha figo yake ilishindwa kufanya kazi.
Mwaka 2008, mguu wake wa kushoto ulikuwa na urefu wa inchi tano kuliko wa kulia na ulikuwa na uzito wenye kilogram 95.
Mwaka 2010 ulikatwa baada ya kupata maambukizi. Hivi sasa ana mguu mmoja ambao hata hivyo nao unazidi kukua na mpaka sasa una uzito wa kilogram 107.
Herieth Makwetta kwa msaada wa mtandao
chanzo : mwananchi
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment