WAZIRI MKUU WA ISRAELI AIOMBA RADHI UTURUKI




Waziri Mkuu wa Israel, Binyamin Netanyahu amesema "anaiomba msamaha" Uturuki kwa kosa lolote lililopelekea kuuawa kwa raia tisa wa Uturuki mwaka 2010 katika msafara wa meli iliyokuwa ikipeleka msaada katika eneo la Gaza.

Netanyahu pia alisema kuwa Israel imekubali kuzifidia familia za waathirika.

Katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, "wawili hao walikubaliana kusawazisha mambo baina ya nchi hizo, ikiwemo kurejesha uhusiano wa kibalozi na kufuta mchakato wa kisheria dhidi ya wanajeshi wa Israeli.”

"Waziri Mkuu Netanyahu aliwaomba msamaha raia wa Uturuki kwa kila kosa linaloweza kuwa limepelekea kupoteza maisha na alikubali kukamilisha makubaliano ya kutoa fidia.”

Ikulu ya Marekani ilisema kuwa Rais Barack Obama amempongeza Netanyahu kwa hatua yake ya kupiga simu na kuomba radhi.

Ripoti zinasema kuwa Waziri Mkuu wa Uturuki, Erdogan, alilikubali ombi la Netanyahu.

Mnamo Mei 31, 2010, Makomando wa Israeli waliuvamia msafara wa meli sita za misaada ya kibinaadami uliokuwa ukielekea katika eneo la Gaza.

Wanaharakati tisa wa Kituruki waliuawa katika meli ya Mavi Marmara, jambo lililoibua lawama ya kimataifa na kusababisha mgogoro wa kidiplomasia baina ya Israeli na Uturuki.
 
Uchunguzi uliofanywa kuhusu tukio hilo ulisema kuwa Israeli ilivunja sheria ya kimataifa na haki za kibinaadamu.

Uchunguzi huo ambao baadaye uliungwa mkono na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binaadamu, ulipata “ushahidi wa wazi unaounga mkono mashitaka” ya uhalifu ikiwemo “ kuua kwa makusudi; kutesa au matendo yaliyo kinyume na ubinadamu; kusababisha mateso makubwa kwa kukusudia au kuujeruhi vibaya mwili au kuathiri afya.”

Israel imeuweka Ukanda wa Gaza chini ya kizuizi tangu Juni 2007 baada ya kundi la Hamas kulidhibiti eneo hilo.

Japokuwa vikwazo vya Israeli vimepunguwa, wananchi wa Gaza wana uhuru mdogo sana wa kutembea, nab ado Israeli imezuia meli yoyote kuingia katika eneo hilo.

CHANZO: ALJAZEERA
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment