WAPIGANAJI WA AL-SHABAB WAUDHIBITI MJI KUSINI MWA SOMALIA


The file photo shows al-Shabab fighters standing guard in their military base in an unknown location in Somalia.
Wapiganaji wa Al-Shabab



Wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia wameudhibiti mji wa kusini wa Hudur baada ya wanajeshi wa Ethiopia kuondoka, hayo ni kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa mji huo.


“Hudur (katika eneo la kusini la Bakool la Somalia) sasa hivi uko chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Al-Shabab baada  ya wanajeshi wa Ethiopia kuondoka usiku wa jana," alisema mkazi mmoja.

 

Mkazi mwingine alisema kuwa “wanajeshi wa serikali ya Somalia nao pia waliondoka pamoja na wanajeshi wa Ethiopia, na baadhi ya raia waliohofia maishayao."


Kadhia hii inakuja baada ya tarehe 27 Februari majeshi ya Umoja wa Afrika pamoja na vikosi vya serikali ya Somalia kuudhibiti mji wa Burhakaba, ambayo ilikuwa ngome ya wapiganaji wa al-shabab. Mji huu muhimu upo kilometa 190 (maili 120) kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Mwezi Desemba 2006, al-Shabab walianza jaribio la kuiangusha serikali ya zamani ya mpito.
 

Katika mchakato huo, wapiganaji wa al-Shabab walikabiliana na wanajeshi wa Ethiopia walioingia Somalia katika kile kinachoitwa kuwa ni kazi ya kuisaidia serikali.
 

Mnamo Agosti 2012, serikali ya shirikisho ya Somalia ilichukua nafasi ya serikali ya mpito, ambayo ilishindwa kuyadhibiti makundi yenye silaha na kurejesha amani licha ya kupsta msaada kutoka serikali za Afrika na Ulaya.

Kundi la al-Shabab limeapa kuiangusha serikali ya Rais Hassan Sheikh Mohamud, aliyeingia madarakani mnamo Septemba, 2012 baada ya kuchaguliwa na bunge jipya la nchi hiyo. 

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment