Mchungaji aliyetorosha watoto asomewa mashitaka hospitali

na Charles Ndagulla, Moshi

DANADANA za kutofikishwa mahakamani kwa Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Jean Felix Bamana (45) anayetuhumiwa kuwasafirisha watoto wawili ndugu na kuwaficha jijini Dar es Salaam jana zimegonga mwamba baada ya kusomewa mashitaka yanayomkabili akiwa hospitali.

Mchugaji huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alisomewa mashitaka hayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Mawenzi) baada kugoma kupelekwa mahakamani tangu Jumatatu wiki hii akidai ni mgonjwa huku askari wanaomlinda wakilalamika kuwa anafanya mchezo wa kuigiza.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Naomi Mwerinde, wakili wa serikali Stella Majaliwa, alidai kuwa Februari 18 mwaka huu huko Masama Wilaya ya Hai mchungaji huyo anadaiwa kuwasafirisha watoto hao (majina yamehifadhiwa) kwenda jijini Dar es salaam.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na kunyimwa dhamana kutokana na mashitaka anayokabiliana nayo kutokuwa na dhamana kisheria na kesi hiyo kuahirishwa hadi Machi 27 mwaka huu itakapotajwa kwani upelelezi wake haujakamilika.

chanzo : mtanzania

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment