KONGO YAZIMA NJAMA YA KUMUUA RAIS JOSEPH KABILA

Congolese President Joseph Kabila
Rais wa Kongo Joseph Kabila




Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo imesema kuwa imezima njama ya mauaji inayomhusisha mbunge mmoja kutoka Ubelgiji dhidi ya Rais Joseph Kabila.


Jana ijumaa, Waziri wa mambo ya ndania, Richard Muyej alisema kuwa wahusika, daktari wa Kibelgiji Jean-Pierre Kanku Mukendi na afisa wa zamani wa jeshi la Polisi ya Kongo Isidore Madimba Mongombe, walitiwa nguvuni mwezi Februari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa, shirika la habari la Reuters limeripoti.


Muyej aliongeza kuwa wawili hao walikiri kupanga njama ya kumuua Rais Kabila mwenye umri wa miaka 41 na kuiangusha serikali yake.

"(Mukendi) alikiri kuwa mpango wa kuushambulia mji wa Kinshasa na kumuondosha rais wa nchi ulifikiwa katika kikao kilichoongzwa na yeye mwenyewe tarehe 20 Januari mjini Kinshasa,” alisema.


Waziri huyo alisema kuwa Mukendi, kwa kusaidiwa na Mbunge wa Bunge la Wawakilishi la Ubelgiji, walitengeneza kundi waliloliita "Mouvement Debout Congolais", yaani Vuguvugu la kuiinua Kongo.

"Kwa kusaidiwa na Mbunge wa Ubegiji, Laurent Louis, alifanya vikao vya siri na raia wa Kongo wanaoishi Ubelgiji kwa lengo la kuandaa na kukamilisha mpango wao wa kuziondosha taasisi za Kongo," alisema.

Kabila aliteuliwa na kikao cha ndani kuiongoza Kongo baada ya baba yake, Laurent Kabila, kuuawa mwaka 2001. Alichaguliwa kuwa rais wa taifa hilo kubwa lenye utajiri wa madini mwaka 2006 na 2011.

Kongo imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiafrika. Changamoto hizo ni pamoja na umaskini, miundombinu mibovu na vita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo vilivyozuka mwaka 1998 na kupoteza maisha ya watu milioni 5.5.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment