
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamesema kiasi cha
watoto milioni 30 kusini mwa jangwa la Sahara hawaendi shule kwa sababu ya
umaskini na mizozo ya kivita inayolikumba bara la Afrika.
Takwimu hizo mpya zimetolewa katika ripoti mbili
zilizochapishwa jana Jumanne na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia
watoto (UNICEF) na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO).
Kwa mujibu wa takwimu za UNESCO, kiasi cha watoto
milioni 19 hawapati elimu ya msingi katika nchi za Magharibi na Katikati mwa
bara la Afrika, huku kiasi cha watoto milioni 10 katika maeneo ya kusini na
mashariki mwa Afrika wakikosa shule.
Ripoti hizo za UNICEF na UNESCO zinasema kuwa mgogoro wa
kiuchumi duniani na mizozo ya vita barani Afrika vinafifiza juhudi za
kuwarejesha watoto hao shuleni. Katika maeneo yenye vita mazingira yamekuwa
hatari zaidi kwa watoto kufika shuleni.
0 comments:
Post a Comment