Rais wa Marekani Barack Obama |
Mtu mmoja kutoka Mississippi aliyekiri kosa la kutuma
barua zenye sumu kwa Rais Barack Obama na maofisa wengine amehukumiwa kifungo
cha miaka 25 jela.
James Everett Dutschke alikiri kutenda kosa hilo mwezi
Januari kwamba aliwatumia barua zenye sumu kali Rais Obama, Seneta wa Mississippi
Roger Wicker na Jaji Sadie Holland. Baadaye
aliikana kauli yake, lakini wiki iliyopita aliirejea tena ili kukwepa adhabu ya
kifo kama angekutwa na hatia.
Aidha, Dutschke atatumikia adhabu ya kifungo cha nje cha
miaka 5 akiwa chini ya uangalizi maalumu atakapotoka gerezani. Wakati huo
atakuwa na umri wa miaka 66.
0 comments:
Post a Comment