askari wa zimamoto na wananchi wa kawaida wakiwa wamekusanyika katika eneo la tukio mjini Baghdad. |
Kwa uchache watu kumi na mbili wameuawa na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu jirani na msikiti kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Shirika la habari la AP limeripoti kuwa, dakika chache baada ya shambulizi la Kanaan, bomu jingine liliripuka jirani na msikiti wa wafuasi wa madhehebu ya Shia magharibi mwa Baghdad na kujeruhi watu 8.
Mashambulizi haya yanakuja kabla ya uchaguzi wa majimbo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Mnano Aprili 20 katika majimbo 12 kati ya majimbo 18 ya Iraq.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mwezi uliopita watu 271 waliuawa, ikiwa ndiyo idadi kubwa kabisa ya vifo kwa mwezi tangu Agosti mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment