LIPUMBA: UKOSEFU WA AJIRA TANZANIA UNATISHIA AMANI




Mwenyekiti Taifa wa chama cha upinzani cha wananchi CUF amesema kuwa, ukosefu wa ajira nchini humo unatishia amani. Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amesema hayo mjini Kigoma katika mkutano wa hadhara wa chama hicho na kusisitiza kwamba, nchi inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa ajira na kutahadharisha kwamba, ukosefu wa ajira unatisha, na ikiwa vijana hawana ajira wanaweza kushawishika kufanya jambo lolote ambalo linaweza kuliletea madhara Taifa.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa katiba, Prof. Lipumba ametaka katiba mpya ijayo itamke wazi kuwa maliasili za Tanzania ni mali ya Watanzania na iweke utaratibu ambao Watanzania wataweza kunufaika na rasilimali hizo.

 Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika mkutano huo amesema, chama cha CUF kitasimamia sera yake ya haki na usawa, ili kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata haki zake za msingi zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na huduma za jamii.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment