Utafiti mpya umeeleza kuwa mazoezi ya ‘yoga’ yanaweza
kuwasaidia watu kupungumza hatari ya vyanzo vya maradhi ya moyo, hususan kama
hawawezi kufanya aina nyingine ya mazoezi yanayotumia nguvu.
Utafiti huo mpya uliochapishwa jana katika Jarida la European
Journal of Preventive Cardiology ulibaini kuwa yoga ina faida na manufaa
muhimu, ikiwemo kushusha kiwango cha hatari ya unene wa kupindukia, shinikizo
la damu na kolesteroli iliyozidi.
Watafiti hao walikuwa wamechambua tafiti 37 za mwanzo
zilizowahusisha watu wapatao 3,000 nchini Uholanzi.
Mtafiti Myriam Hunink, kutoka kituo cha Afya cha Chuo
Kikuu cha Erasmus mjini Rotterdam, anasema kuwa “Yoga ina faida za kupunguza
vyanzo vya hatari sawa na faida zinazopatikana katika mazoezi ya kukimbia au
kuendesha baiskeli.”
Maureen Talbot, muuguzi mwandamizi katika Taasisi ya
Moyo ya Uingereza anasema kuwa faida za Yoga “zinaweza kuwa zinatokana na
ufanyaji kazi wa misuli na kupumua, ambapo inaweza kuingiza hewa nyingi ya ‘oxygen’
mwilini, jambo linaloweza kupunguza shinikizo la damu.”
Yoga ni aina ya mazoezi ya kale yenye asili ya India
takribani miaka 5,000 iliyopita. Mazoezi hayo hujumuisha mikao maalumu ya
mwili, mazoezi ya kupumua, mbinu za kupumzika na kutafakari, na inahusishwa na
faida nyingine nyingi za kiafya.
0 comments:
Post a Comment