ASKARI WA NIGERIA WAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO

The file photo shows a Nigerian court martial.
Mahakama ya kijeshi nchini Nigeria (picha ya maktaba)


Mahakama ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu askari 54 adhabu ya kifo kwa kukataa kupigana na wanamgambo wa kundi la Boko Haram huku askari wengine watano wakiondolewa mashtaka.

Imeripotiwa kuwa askari waliotiwa hatiani walikataa kushiriki operesheni ya kijeshi mwezi Agosti iliyolenga kuikomboa miji mitatu inayoshikiliwa na Boko Haram.

Mwezi Septemba askari 12 walipewa adhabu ya kifo kwa kile ambacho mahakama ilisema kuwa ni uasi na jaribio la kumuua kamanda wao wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo hao.

Kundi la Boko Haram limedai kuhusika na mashambulizi kadhaa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo tangu lilipoanzisha uasi wake mwaka 2009. Mpaka sasa zaidi ya watu 10,000 wameshapoteza maisha katika mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa wakimbizi, Wanigeria wapatao 650,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya kundi hilo na wamegeuka kuwa wakimbizi wa ndani, huku maelfu ya watu wakikimbilia katika mataifa jirani.


Kundi la Boko Haram – ambayo ina maana ya “elimu ya Kimagharibi ni haramu” – linasema kuwa lengo lake ni kuiondosha madarakani serikali ya Nigeria.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment