HUYU NDIE MWANAMKE MFANYAKAZI WA BENKI ALIYEIBA SAHIHI ZA WATEJA 150 NA KUWAUZIA WAHALIFU.

Afisa wa benki ya NatWest alishtakiwa kwa kosa la kuuza taarifa za wateja kwa kundi la wahalifu ambapo amehurumiwa kufungwa gerezani kwasababu ana watoto wadogo wawili.
Lekeshia Henry-Richards, 28, aliiba sahihi za wateja 150 waliokuwa wakitumia huduma binafsi katika jiji la London.
Taarifa hizo zilitumika kuwaibia wateja ambapo wateja kadhaa wameibiwa kupitia kundi hilo la kihalifu kabla ya ishu nzima kugundulika April mwaka huu na mwanamke huyo kufikishwa mahakamani.
Mwanamke huyo kutoka Leytonstone, Mashariki mwa London alisamehewa kufungwa gerezani kwasababu ana watoto wadogo wawili mmoja mwenye miaka minane na mwingine miezi 18.
Alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani na kuagizwa kufanya kazi kwa saa 90 bila malipo.
Share on Google Plus

About www.habarika24.blogspots.com

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment