SULLEY MUNTARI AONDOLEWA KATIKA KIKOSI CHA BLACK STARS






Chama cha Soka cha Ghana  (GFA) kimemsimamisha mara moja Sulley Ali Muntari bila kikomo kushiriki katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, Black Stars.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kitendo cha Muntari kumshambulia kwa makusudi Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama hicho na Mjumbe wa Menejimenti ya Black Stars, Bwana Moses Armah siku ya Jumanne tarehe  24 Juni, 2014 wakati wa kikao.

Ushiriki wa Muntari katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 umesitishwa mara moja.

Chanzo: Ghanafa.org
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment