JONATHAN: BOKO HARAM HAWATAKWAMISHA UCHAGUZI

Rais wa Nigeria, Goodluck Ebele Jonathan

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amewahakikishia Wanigeria kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika kama ulivyopangwa licha ya changamoto za kiusalama zinazoikumba nchi hiyo.

Akizungumza jana katika kanisa moja mjini Abuja, Rais Jonathan alisema kuwa serikali yake inaendelea na mikakati yake ya kimaendeleo na kisiasa licha ya changamoto hizo na kwamba uchaguzi huo wa urais na ubunge utafanyika katika mazingira mazuri ya kidemokrasia na uhuru.

Aidha, Rais Jonathan amesisitiza kuwa programu za mageuzi zinazotekelezwa na serikali yake sio programu hewa bali zimeanza kutoa matunda ya kujivunia katika sekta muhimu kama vile kilimo, miundombinu, nishati, viwanda na makazi.


Rais Jonathan aliwataka wananchi kuomba na kusali ili kufanikisha juhudi za kuwakomboa wasichana zaidi ya 200 wanaodaiwa kutekwa na kundi la Boko Haram.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment