Wanavijiji wa Afghanistan wakiwa wamekusanyika kwenye
eneo yalipotokea maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Argo katika jimbo la
Badakhshan, Mei 2, 2014.
|
Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko makubwa
ya ardhi katika jimbo la Badakhshan kaskazini mashariki mwa Afghanistan
imefikia zaidi ya watu 2,100, huku zoezi la kutafuta manusura likiendelea.
Msemaji wa gavana wa jimbo hilo amesema kuwa watu 2,100 kutoka
katika familia 300 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 4,000
wamekosa makazi kutokana na janga hilo.
Taarifa kutoka huko zinasema kuwa wanavijiji wameungana
na vikosi vya polisi kuwatafuta manusura huku wakitumia zana duni.
Mamia ya makazi yameharibiwa vibaya sana na maporomoko
ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa katika eneo
hilo.
Eneo hilo limekuwa likikumbwa na matukio ya maporomoko
ya ardhi katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mashirika ya misaada ya kimataifa, Afghanistan
ni eneo lenye matukio mengi ya majanga ya asili, ambayo huathiri maisha ya maelfu
ya watu kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment