Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha ( AICC ).
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini baadhi ya hati za makubaliano ya Jumuiya hiyo. Kutoka kulia ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Uhuru Kenyata, Rais wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyeta wa Kenya akihutubia Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.
Viongozi wa Mtaifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua Mnara wa kumbumbuku ya mauaji ya Rwanda yaliyotokea taktibani miaka ishirini iliyopita hapo Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha Tanzania. Kutoka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Uhuru Kenyata, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana PierreDamieni Habumuryemi.
Wakuu waJumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo jijini Arusha Tanzania. Kutoka kushoto waliokaa vitini ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais Dkt Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
(Kupitia Michuzi blog)
0 comments:
Post a Comment