Moshi mkubwa ukifuka baada ya bomu lililolipuka kwenye kambi ya jeshi la Libya mjini Benghazi leo Aprili 29, 2014. |
Mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye gari katika kambi ya
jeshi kwenye mji wa Benghazi nchini Libya umeua askari wawili.
Maafisa nchini humo wanasema kuwa mlipuko huo umetokea
kwenye lango la kambi ya vikosi maalumu jirani na uwanja wa ndege wa mji huo.
Hata hivyo, hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na
shambulizi hilo.
Mji wa Benghazi umekuwa ukishuhudia matukio mengi ya
mashambulizi na mauaji ya kisiasa kutokana na makundi ya waasi waliomng’oa
Kanali Muammar Gaddafi kuingia katika vita vya kugombania madaraka.
Mnamo Machi 17, askari kumi waliuawa katika mfululizo wa
milipuko ya mabomu ya kutegwa kwenye magari ambayo iliitikisa kambi moja ya
jeshi katika mji huo.
Mwezi mmoja baadaye, watoto kumi na mbili walijeruhiwa
katika mlipuko ndani ya ndani ya shule moja mjini Benghazi baada ya mtu mmoja
aliyekuwa kwenye hari kurusha bomu katika shule hiyo.
Miaka mitatu baada ya kuanguka kwa Kanali Gaddafi, nchi
hiyo bado imeendeea kukumbwa na hali ya ukosefu wa usalama baada ya waasi
waliomuondoa Gaddafi kukataa kuweka silaha chini licha ya juhudi za serikali
kuu kujaribu kuweka sheria na kudhibiti hali ya mambo.
0 comments:
Post a Comment