WATU ELFU 10 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA UFILIPINO

A man walks past a tree uprooted by strong winds brought by super Typhoon Haiyan that hit Cebu city, central Philippines on November 8, 2013.
MWananchi akipita jirani na mti uliong'olewa na upepo mkali uliosababishwa na kimbunga Haiyan katika mji wa Cebu, katikati mwa Ufilipino, Novemba 8,2013.





Na Kabuga Kanyegeri


KWA uchache, watu wapatao 10,000 wanahofiwa kupoteza maisha katika jimbo la katikati mwa Ufilipino la Leyte baada ya kimbunga Haiyan kuikumba nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.


Mkuu wa polisi katika jimbo hilo, Elmer Soria, ameseka kuwa kimbunga hicho kiliharibu karibu asilimia  70 mpaka 80 ya eneo hilo wakati kikielekea katika jimbo la Leyte.

Kimbunga Haiyan, ambacho kinasemekana kuwa kimbunga machachari zaidi kuwahi kutokea Ufilipino, kiliangusha majumba, kikasababisha mmomonyoko wa ardhi, mafuriko, kikakata umeme na mawasiliano katika visiwa sita vya nchi hiyo.

Kimbunga hicho kilisababisha vifo vingi na hasara kubwa kwenye kisiwa cha Leyte wakati kilipokuwa kikielekea katikati na kaskazini mwa nchi ya Vietnam.

Maafisa nchini Vietnam wamewahamisha zaidi ya watu 500,000 kutoka katika maeneo yaliyotarajiwa kupitiwa na kimbunga hicho.


Wastani wa vimbunga 20 huipiga nchi ya Ufilipino kila mwaka. Mwezi Desemba mwaka 2011, Kimbunga Washi kilisababisha vifo vya watu 1,200, kuwahamisha watu 300,000 na kuyaharibu zaidi ya makazi 10,000.

Mwaka jana kimbunga Bopha kilipiga katika miji mitatu ya pwani kwenye kisiwa cha Mindanao, kikaua watu 1,100 na kusababisha uharibifu unaokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani bilioni 1.04.

Mwezi Septemba, Kimbunga Usagi, kilichokuwa kikisafiri kwa kasi ya kilometa 240 kwa saa, kilipiga katika kisiwa cha Batanes kilichopo kaskazini mwa nchi hiyo kabla ya kusababisha hasara kubwa nchini China.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment