![]() |
| baada ya kufikishwa hospitali ya Mhimbili |
![]() |
Dkt. Sengondo Mvungi, amejeruhiwa vibaya sehemu za
kichwani na usoni, baada ya kukatwa mapanga, nyumbani kwake, Kibamba Msakuzi, nje
kidogo ya jiji, majira ya saa sita usiku Jumamosi Novemba 2, 2013.
|
Kwa mujibu wa taarifa za ndugu na polisi, Dkt. Mvungi
ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, mkoani
Pwani, alicharangwa mapanga, baada ya kutaka kujua nini kilichokuwa kikiendelea
kufuatia mabishano baina ya mkewe na watu hao ambao walitishia kumuua endapo
asingewapa fedha.
Taarifa zinasema, watu hao sita wengine wakiwa nje ya
nyumba kwa nia ya kujihami endapo wangevamiwa na majirani, walivamia nyumba
hiyo yenye ghorofa moja, na kumkuta mkewe Dkt. Mvungi wakati huo Dkt. Mvungi
akiwa kwenye chumba tofauti katika nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wavamizi walipoona mke wa
Dkt. Mvungi anachelewa kutekeleza maagizo yao, walifyatua baruti na hapo Dkt.
Mvungi akajaribu kuelekea kulikotokea mlio huo na ndipo alipokutana na mapanga
ya kichwani na usoni.
Uchunguzi wa awali wa polisi umeonyesha kuwa tukio hilo
ni la kihalifu, kwani watu hao ambao kwa sasa wanatajwa kama majambazi, waliiba
fedha, simu na laptop, hali inayoonyesha wazi kuwa nia yao ilikuwa ni
kutekeleza wizi.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.


0 comments:
Post a Comment