Watu waliohamishwa kwenye makazi yao wakisubiri
katika ukumbi wa Westfalen Halle mjini Dortmund, Ujerumani leo Jumapili Nov. 3,
2013.
ZAIDI ya watu 20,000 wameondolewa katika makazi yao
katika mji wa Dortmund, magharibi mwa Ujerumani, wakati mamlaka zikijiandaa
kutegua bomu kubwa lililoachwa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Bomu hilo lenye uzito wa kilogramu 1,800
liligunduliwa baada ya wataalamu kuzichambua picha mbalimbali zilizopigwa na
ndege maalumu iliyokuwa ikitafuta silaha zilizodondoshwa na majeshi ya
Washirika kwenye eneo la viwanda la mkoa wa Ruhr nchini Ujerumani.
Bomu kama hilo lililopatikana miaka miwili iliyopita
lilipelekea kuhamishwa kwa watu wapatao
45,000 katika mji wa Koblenz karibu na mto Rhine.
CHANZO: Global News
0 comments:
Post a Comment