Mwishoni mwa juma hili kumekuwepo na sintofahamu mjini Nairobi,
nchini Kenya, baada ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 kukamatwa. Kwa
muda mrefu kijana huyo amekuwa akiwadanganya wanaume wenzake kwa kujifanya kuwa
ni mwanamke.
Mwanaume huyo alitengeneza matiti ya bandia ambapo
alichukua glovu mbili na kuzijaza maji kisha akazipakachika vizuri ndani ya
sidiria. Alivaa kama mwanamke na kuonekana mwenye mvuto kwa kuwa alikuwa
ameyatengeneza makalio yake katika namna iliyowavutia wanaume.
Kwa mujibu wa wenzake, mtu huyo amekuwa akifanya hivyo
kwa muda sasa na hawakuwahi kumshuku hata kidogo. Alionekana kama mwanamke na
muda wote alivaa vizuri na kuwa na muonekano maridadi.
Akizungumza na wanahabari, mshukiwa huyo alikiri kwamba
alianza kuvaa kama mwanamke na kufanya ukahaba tangu mwaka jana.
Alidai kuwa alikuwa akiikimu familia yake kwa hoja
kwamba alitafuta kazi kwa miaka mingi bila mafanikio, hivyo akaamua kujiingiza
katika mchezo huo.
Alisema kuwa alifurahia uhusiano na wanaume wengi na
kwamba anahuzunika kwa kubainika wakati alikuwa anahitaji kuendelea na shughuli
yake.
CHANZO: kenyan-post
0 comments:
Post a Comment