SERIKALI YA KONGO: TUTASAINI MAKUBALIANO YA AMANI NA WAASI JUMATATU

M23 rebels walk through the jungle in the Democratic Republic of Congo
Waasi wa M23 wakiwa msituni katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini Kongo



WAZIRI wa Mashaurı ya Kıgenı wa Jamhurı ya Kıdemokrasıa ya Kongo,  Raymond Tshibanda, amesema kuwa siku ya Jumatatu serikali ya nchi hiyo itasaini makubaliano ya amani na waasi wa kundi la M23.

Mnamo Novemba 5, kundi la M23 lilisema litaweka silaha chini na kufanya mazungumzo ya amani baada ya ngome zake kudhibitiwa na jeshi la Kongo katika milima ya Tshanzu na Runyoni kwenye mpaka wa Uganda na Rwanda.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo, utiaji saini utafanyika katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Waasi wa M23 walijiondoa katika jeshi la Kongo mwezi Aprili 2012 kupinga kile walichodai kuwa ni mwenendo mbaya ndani ya jeshi la Taifa (FARDC). Walikuwa wamejumuishwa katika jeshi chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2009.

Tangu mwezi Mei 2012, takriban watu milioni 3 wameyekimbia makazi yao katika eneo la mashariki mwa Kongo. Takriban watu milioni 2.5 ni wakimbizi wa ndani, huku zaidi ya watu 460,000 wamekimbilia katika nchi za Rwanda na Uganda.


Kongo imekuwa ikikabiliwa na matatizo matatizo kwa miongo kadhaa, kama vile umaskini uliokithiri, miondombinu mibovu, na vita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambavyo viliibuka tangu mwaka 1998 na kugharimu maisha ya zaidi ya watu milioni 5.5.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment