MSAFARA WA HARUSI WASHAMBULIWA, BWANA HARUSI AUAWA


 


Watu wenye silaha wameushambulia msafara wa harusi katika, nchini Nigeria na kuua zaidi ya watu 30, kwa mujibu wa mashuhuda na manusura.

Msemaji wa serikali ya jimbo la Amadawa, Ahmad Sajo amesema kuwa sherehe ya harusi ilifanyika katika kijiji cha Fugi, ambapo bwana harusi na wageni mbalimbali walikuwa wakielekea nyumbani ndipo waliposhambuliwa kwenye barabara kuu kati ya miji ya Bama na Gwoza katika jimbo jirani la Maiduguri. Barabara hiyo hupitia kwenye misitu inayojulikana kuwa maficho ya waasi na makundi mbalimbali yenye silaha.

Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika, ingawa serikali inalitupia lawama kundi la Boko Haram, ambalo linadaiwa kujihusisha na matukio kama hayo.

Wiki iliyopita, kundi hilo lilikishambulia kizuizi cha jeshi kwenye barabara hiyo na mashuhuda wanasema kuwa kwa uchache askari 4 wa serikali waliuawa.


Mashambulizi mbalimbali yamekuwa yakiendelea licha ya jeshi kuwafukuza waasi hao katika miji mikubwa ya eneo la kaskazini mashariki huku maeneo hayo yakiwa chini ya hali ya hatari iliyotangazwa miezi mitano iliyopita.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment