WATUHUMIWA WA UGAIDI MSITUNI WALIVYOPELEKWA MAHAKAMANI LEO MTWARA



Polisi walijua kabisa msafara wao utakua umewabeba watuhumiwa waliokamatwa kwenye mafunzo ya kijeshi ambayo yalikua yanatolewa kupitia CD za Al Qaeda na Al Shabaab hivyo wakajiandaa kwa ukubwa huu
Maandalizi ya Jeshi Polisi yalivyokuwa


Watuhumiwa wa ugaidi waliokamatwa wakifanya mazoezi msituni mkoani  Mtwara, walipelekwa Mahakamani asubuhi ya leo Oktoba 17 2013 lakini kutokana na baadhi ya taratibu za kimahakama ikashindikana kupandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mtwara hivyo wakarudishwa mahabusu mpaka hapo itakapoamuliwa ni siku gani wapelekwe tena Mahakamani.

Mwanzoni walikua wamekamatwa 11 tu lakini taarifa nyingine zinadai kwamba idadi imeongezeka baada ya wengine wawili kukamatwa kulekule walikokamatiwa wengine ambapo hawa wawili hawakukutwa na silaha wala kingine chochote kama ilivyotokea kwa wale wa mwanzo ambao walikutwa na mapanga, silaha mbalimbali pamoja na CD za DVD ambazo zinamafunzo ya kijeshi ya Al Shabaab na Al Qaeda.


Wawili hawa wamekiri kwamba mwalimu wao kule msituni alikua akiwapa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo kupiga karate, utumiaji wa silaha ambapo pia walikua wakiishi hukohuko msituni kwenye Mapango.


5


2



7

8


9
Gari lililowabeba watuhumiwa


1

2


PICHA KWA HISANI YA milllardayo.com

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment