SHABIKI maarufu wa Yanga, Steven Mwamwala amedai kuwa,
kama wakifungwa na Simba mechi ya Jumapili ijayo itakayochezwa Uwanja wa Taifa,
atajinyonga.
Na akamsisitizia mcheza filamu, Wema Sepetu afike
uwanjani kuona mechi ya Simba na Yanga Jumapili ili ampe zawadi yake ya jezi ya
Yanga aliyoigharamia Sh45,000.
Mwamwala ana historia na Yanga ilipopigwa mabao 5-0
aliangua kilio cha nguvu na video zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli ya shabiki huyo inakuwa mzigo kwa wachezaji wa
Yanga kama, Athuman Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani, Mrundi Didier Kavumbagu na Wanyarwanda Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima
‘Fabregas’ kuhakikisha wanafanya vizuri na kuokoa maisha ya kijana huyo mwenye
miaka 31.
Aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Nimeandaa kamba ya katani
kabisa, nimeificha na siwezi kusema nilipoiweka kama Yanga itafungwa mchezo
huo, nitajinyonga ili kupoteza uhai wangu. Unajua inauma sana mnapofungwa,
nataka timu yangu ishinde Jumapili ili niwe na amani kwa ushindi wowote ule
ilimradi tutoke na pointi tatu.”
Kuhusu, Wema shabiki huyo alisema anampenda sana kama
dada yake na anatamani akutane naye.
“Nimemtafuta sana na naomba siku hiyo aje kwa sababu
nimemwandalia zawadi. “Nimemnunulia jezi ya Yanga na tayari nimeiandika jina la
Wema, imenigharimu Sh 45,000,” alifafanua Mwamwala ambaye anaishi Tabata
Segerea jijini Dar es Salaam.
CHANZO: Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment