Gari lililobeba milipuko limelipuka jirani na ubalozi
mdogo wa Sweden katika mji wa mashariki wa Benghazi nchini Libya, ingawa hakuna
majeruhi walioripotiwa.
Maafisa usalama wa Libya wamesema leo kuwa mlipuko huo
uliliharibu vibaya sana jengo la ubalozi huo uliopo katika wilaya ya al-Fouihet
mjini Benghazi.
“Mlipuko mkubwa uliotokea mbele ya ubalozi mdogo wa
Sweden ulisababisha uharibifu mkubwa kwenye jengo hilo na kwenye majengo ya
jirani lakini hakuna vifo vilivyotokea,” alisema Kanali Abdullah Zaidi.
Mwezi Agosti, ubalozi mdogo wa Misri katika mji huo
ulishambuliwa na watu wasiojulikana waliorusha vifaa vya milipuko kwenye jengo
hilo na kusababisha uharibifu mkubwa.
Shambulizi baya zaidi lilitokea Septemba 2011, baada ya
watu wenye silaha kuushambulia ubalozi mdogo wa Marekani mjini humo na kumuua
abalozi Chris Stevens na kuwajeruhi Wamarekani wengine watatu.
0 comments:
Post a Comment