Rais wa shirikisho la soka Tanzania -TFF Leodgar Tenga
ameapa kuwa ni lazima uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo kufanyika kama
ulivyopangwa Oktoba 27 licha ya baadhi ya wadau kutishia kuusimamisha kwa madai
ya kutoridhika na uamuzi wa kuondolewa katika kinyang'anyiro hicho.
Rais Tenga amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uchaguzi huo ambao awali uliingia dosari
baada ya shirikisho la soka la kimataifa FIFA kuagiza kusitishwa kwa mchakato
huo na kutaka kuundwa kwa kamati za maadili baada ya kupokea malalamiko kutoka
kwa wagombea walioenguliwa.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mwezi Februari
mwaka huu ambapo rais Tenga amesema dhamira ya TFF ni kuona uchaguzi huo
unakuwa huru na wa haki na kuongeza kuwa mchakato wa uchaguzi huo sasa
unakwenda vizuri tangu FIFA ilivyoagiza kuanza upya.
0 comments:
Post a Comment