MRITHI WA SHEIKH ABOUD ROGO NA WENZAKE 3 WAUAWA





Watu ambao hawajabainishwa wamempiga risasi na kumuua kiongozi wa Kiislamu aliyeuawa Sheikh Aboud Rogo, Sheikh Ibrahim Rogo pamoja na wenzake watatu usiku wa kuamkia leo.

Sheikh Ibrahim Rogo na wenzake wanne walikuwa wakielekea nyumbani kutoka Masjid Musa kwa ajili ya ibada ndipo gari yao ilipomiminiwa risasi zilizowaua wanne kati ya watu waliokuwa katika gari hiyo kwenye umbali wa nusu kilometa kutoka kituo cha polisi cha Bamburi.

Wengine waliokuwa katika hiyo gari ni bwana Gadaffi Muhammad anayesemekana kuwa fundi seremala, bwana Issa Abdalla shemeji wa Gadaffi na ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha hiyo gari, Omar Abu Rumeisa na Salim Aboud ambaye alipona kimaajabu katika shambulizi hilo baada ya kujifanya kuwa amekufa.

Salim Aboud anasema kuwa walikuwa wakielekea nyumbani katika gari aina ya a Toyota Fun Cargo ndipo watu waliokuwa wakitembea walianza kuishambulia gari yao kwa risasi na kuacha njia.

“Tumewamaliza,” Bwana Salim Aboud aliwasikia wakisema baada ya yeye kujifanya kuwa amekufa. Wauaji wanasemakana kutumia gari aina ya Mrak X kutoka katika eneo hilo.

Viongozi kadhaa wa Kiislamu, akiwemo Sheikh Abubakar Sheriff anayejulikana kwa jina la Makaburi ambaye alifika katika eneo hilo baada ya tukio, alikinyooshea kidole Kikosi Maalumu cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi kuwa ndicho kilichohusika na mauaji hayo.


“Kikosi cha ATPU kilikuwa hapa, kwa nini wamekimbia? Tumefanya nini na kwa nini wanatuua? Hatujamuua yeyote lakini polisi wanawaua Waislamu wasiokuwa na hatia,” alisema Sheikh Makaburi.


“Vitendo hivi vinaongozwa na Wamarekani na Waisraeli, Sheikh Ibrahim hakuwa katika Jengo la Westgate wakati wa shambuli kwenye jengo hilo. Serikali za Kimagharibi hawataki Waislamu wazungumzie Jihad. Jihad ni sehemu ya Uislamu, tuuweni sote,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment