WAASI WA KIKURDI WAANZA KUONDOKA UTURUKI


A file photo shows PKK militants training at a base in northern Iraq.
Wapiganaji wa PKK wakifanya mazoezi kaskazini mwa Iraq



Kundi la waasi wa Kikurdi (PKK) nchini Uturuki limesema kuwa wapiganaji wake wameanza kuondoka Uturuki kuelekea katika ngome zao kaskazini mwa Iraq.


Hatua hiyo iliyoanza leo Jumatano ni sehemu ya mpango wa amani uliofikiwa kati ya Serikali ya Ankara na kiongozi wa PKK, Abdullah Ocalan mapema mwaka huu.  

Gultan Kisinak, kiongozi wa chama chenye mrengo wa Kikurdi cha (BDP), alisema kuwa kundi la kwanza la wapiganaji hao limeanza kuondoka leo kuelekea mpakani mwa Iraq.


Ocalan, ambaye alikamatwa na vikosi vya Serikali ya Uturuki katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, mwaka 1999, anatumikia kifungo cha maisha katika gereza moja kwenye kisiwa cha Imrali kwa makosa ya kuongoza kikundi cha PKK na kuanzisha mapigano na Serikali ya Uturuki.


Katika taarifa iliyotolewa na kundi hilo mapema Jumanne ya jana, lilisema kuwa zoezi hilo "litaendelea katika utaratibu maalumu uliowekwa."



Kundi la PKK limekuwa likipigania kujitenga kwa eneo la kusini mashariki mwa Uturuki tangu miaka ya 1980. Mgogoro huo umegharimu maisha ya makumi kwa maelfu ya watu.



Wapigana kadhaa wa PKK wanaaminika kuwa wanaishi nchini Uturuki, huku tawi lake la kijeshi likiwa na ngome yake kaskazini mwa Iraq.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment