UTURUKI NA SYRIA: KUTOKA URAFIKI MPAKA UADUI



Wakati Uturuki na Syria zikilaumiana na kutupiana shutuma kuhusu milipuko miwili iliyoua watu 46 katika mji wa mpakani nchini Uturuki, jambo la kujiuliza hapa ni kuwa, ilikuwaje washirika hawa wa zamani kuingia katika uadui mkubwa?

Uturuki inashirikiana mpaka mrefu na aliyewahi kuwa rafiki yake mkubwa, Syria. Kwa sasa mpaka wa nchi hizi mbili umefungwa, na pande zote mbili zinalaumiana kuhusu tukio la mlipuko uliotokea juzi Jumamosi kwenye mji wa Reyhanli, Uturuki.


Officers work on May 12, 2013 on a street damaged by a car bomb explosion which went off on May 11 in Reyhanli in Hatay, just a few kilometres from the main border crossing into Syria (AFP Photo / Bulent Kilic)
Maafisa wakifanya kazi kwenye mtaa ulioharibiwa vibaya na mlipuko wa bomu lililotokea Mei 11 katika mji wa Reyhanli, kilometa chache kutoka eneo kuu la mpaka wa Uturuki na Syria. 


Uturuki iliituhumu Syria kuhusika na shambulizi hilo, huku serikali ya Syria ikikanusha na kupinga vikali na kuhusika kwake, na ikasema kuwa shambulizi hilo linatumika kuhalalisha uingiliaji kutoka nje unaofanywa dhidi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu alidai kuwa wale walihusika na mashambuli hayo walitoka katika "kundi la kigaidi la Wamarxisti wa zamani"  wenye mafungamano na serikali ya Assad. "Ni wakati sasa kwa jamii ya Kimataifa kuchukua hatua ya pamoja dhidi ya utawala huu,”  alisema jana Jumapili wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari.

Waziri wa Habari wa Syri, Omran al-Zoubi alitupilia mbali tuhuma na shutuma za Uturuki: “Hakuna mwenye haki ya kuzusha tuhuma za urongo…Syria haijafanya na kamwe haitafanya kitendo kama hicho kwa sababu tunu zetu hazituruhusu kufanya hivyo.”

Lakini, kwa nini hali hii, wakati hapo zamani nchi hizi mbili zilikuwa na uhusiano madhubuti na wa kirafiki baina yao?

 Ni vigumu kuamini hali iliyo kwa sasa, lakini mwaka 2009 nchi hizi mbili zilifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika mpaka huo, jambo linaloonesha ni kwa kiwango gani nchi hizi zilivyokuwa na uhusiano imara na madhubuti.

Syrian President Bashar al-Assad (L) during a meeting with Turkish Foreign Minister Ahmet Davutoglu in Damascus on March 7, 2010 (AFP Photo / Sana)
Rais wa Syria, Bashar al-Assad (kushoto) alipokutana na Waziri Mkuu wa Mashauri ya Kgeni wa Uturuki, Ahmet Davutoglu mjini Damascus Machi 7, 2010.


Mwaka 2003, mataifa haya mawili yalisaini makubaliano ya biashara huru baina yao, kuondoa utaratibu wa visa kwa wananchi wa nchi hizo na mikutano kadhaa baina ya marais.


Wakazi wa mikoa ya mpaka katika nchi hizi wana maingiliano ya karibu, wana ndugu katika pande zote mbili na kuhusi kuwa nchi zote mbili ni nyumbani kwao. Lakini sasa, tuhuma na shutuma kali linazoendelea baina ya nchi hizo, zimeufanya uhusiano huo usiwe kama mwanzo.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment