RAIS WA UFARANSA AIDHINISHA RASMI MUSWADA UNAORUHUSU USHOGA KUWA SHERIA




French President Francois Hollande
Rais wa Ufaransa Francois Hollande





RAIS wa Ufaransa, Francois Hollande, ameweka saini rasmi muswada wa unaoruhusu ndoa za ushoga na wapenzi wa jinsia moja kuasili watoto, na kuifanya Ufaransa kuwa nchi ya 14 kuidhinisha ndoa za jinsia moja.



Hollande amesaini muswada huo leo Jumamosi, siku moja baada ya Baraza la Katika kuitupilia mbali changamoto ya kikatiba iliyowasilishwa na upinzani wa mrengo wa kulia mbele ya baraza hilo.


“Nitahakikisha sheria hii inafanya kazi kikamilifu nchini kote, na sitakubali usumbufu wowote dhidi ya ndoa hizi," alisema Hollande.


Mwezi uliopita, bunge la Ufaransa liliupitisha muswada huo baada ya siku kadhaa za mjadala mzito.


Mara baada ya muswada huo kupitishwa na bunge, chama cha upinzania cha mrengo wa kulia,  UMP cha Rais wa zamani wa nchi hiyo, Nicolas Sarkozy kiliwasilisha pingamizi lake mbele ya Baraza la Kikatiba la nchi hiyo. 

Ufaransa imekumbwa na maandamano makubwa dhidi ya muswada wa ndoa za jinsia moja.


Mapema Ijumaa, waandamani wapatao 200 na 300 walikusanyika katikati ya mji mkuu, Paris wakipinga na kulaani hatua ya Baraza la Kikatiba kuupitisha na kumtaka Hollande ajiuzulu.


Wapinzani wa sheria hiyo wamepanga kufanya maandamano mengine makubwa mjini Paris tarehe 26 Mei.



Aidha, makanisa ya Ufaransa yameulaana vikali muswada huo na kusema kuwa ndoa za mashoga ni "fedheha itakayoutikisa msingi mmojawapo katika misingi ya jamii yetu."


Wakati wa kampeni zake za kuwania urais, Hollande aliahidi kuunga mkono muswada huo utakapoletwa mbele yake kwa ajili ya kuufanya kuwa sheria rasmi.



Nchi mbalimbali za Ulaya kama vile, Uholanzi, Ubelgiji, Hispania, Norway, Sweden, Ureno,  Iceland, na Denmark zimeruhusu ndoa za jinsia moja. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment