MAPOROMOKO YAUA WATU 20

Gold miners pass mud along a human chain in an open pit at the Chudja mine in the Kilomoto concession near the village of Kobu in the northeastern Democratic Republic of Congo. (file photo)
Wachimbaji wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Kobu kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.




SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kuwa watu ishirini wamepoteza maisha kufuatia mvu nzito katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa nchi hiyo.



Jana Ijumaa, msemaji wa Serikali, Lambert Mende, alisema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi katika mgodi wa madini jirani na kijiji kimoja katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini.


Mpaka jana Ijumaa, wafanyakazi wa uokozi bado walikuwa wakiwatafuta watu ambao walihisiwa kuwa bado wako hai na kujaribu kutoa miili ya wale ambao waliaminika kuwa wamefariki dunia.



"Bado tunaendelea kuchimba, hivyo idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Serikali ya jimbo inasimamia shunguli ya uokozi," alisema Mende. 



Majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Kivu Kusini yana hazina kubwa ya madini ya thamani ambayo hutumika katika nchi za Magharibi kutengenezea simu za mkononi, kompyuta na michezo.



Makundi kadhaa yenye silaha, ikiwemo M23, wanaendesha harakati zao za uasi mashariki mwa Kongo na wanapigania kuidhibiti nchi hiyo kubwa yenye maliasili za madini, kama vile dhahabu, urani, coltan, ambayo hutumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya elektroniki, ikiwemo simu za mkononi.

Waasi wa M23 waliuteka mji wa Goma Novemba 20, 2012 baada ya walinda amani kuondoka  katika mji huo wenye wakazi milioni moja. Wapiganaji wa M23 waliondoka katika mji huo Desemba 1,2013 baada ya makubaliano ya kusimamisha mapigano.

Waasi wa M23 walijiondoa katika jeshi la Kongo mwezi Aprili 2012 kupinga kile walichodai kuwa ni mwenendo mbaya ndani ya jeshi la Taifa (FARDC). Walikuwa wamejumuishwa katika jeshi chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2009.

Tangu mwezi Mei 2012, takriban watu milioni 3 wameyekimbia makazi yao katika eneo la mashariki mwa Kongo. Takriban watu milioni 2.5 ni wakimbizi wa ndani, huku zaidi ya watu 460,000 wamekimbilia katika nchi za Rwanda na Uganda.

Kongo imekuwa ikikabiliwa na matatizo matatizo kwa miongo kadhaa, kama vile umaskini uliokithiri, miondombinu mibovu, na vita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambavyo viliibuka tangu mwaka 1998 na kugharimu maisha ya zaidi ya watu milioni 5.5.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment