ASKARI WA TANZANIA WAWASILI MASHARIKI MWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO


Tanzanian soldiers in the eastern Democratic Republic of Congo (file photo)


Kikosi machachari cha askari wapatao 100 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kiwasili nchini Kongo kuungana na kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kukabiliana na makundi yenye silaha katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.



Kwa mujibu wa msemaje wa ujumbe wa kulinda amani Luteni Kanali Felix Basse, kikosi cha  Tanzania kilichowasili mashariki mwa Kongo siku ya Jumamosi, ndiyo kundi la kwanza linalounda kikosi kipya madhubuti cha askari 3000 kuwahi kuundwa na Umoja wa Mataifa kuingilia katika mgogoro katika nchi hiyo ya Kiafrika.



Mnamo Machi 28, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio, ambalo, sio tu liliongeza muda wa ujumbe wa kulinda amani nchini Kongo, bali pia liliunda kikosi maalumu ambacho kitapambana na makundi yenye silaha, badala ya kuwalinda tu raia.



Tarehe 23 Aprili, kamanda wa kikosi hicho aliwasili mjini Goma, lakini askari wenyewe waliokuwa wamepangiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi Aprili ndio kwanza wameanza kuwasili.



Mnamo Mei 4, Kundi la waasi wa M23 liliiambia Tanzania kuwa watayashambulia majeshi yake kama yatajiunga katika kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa.



"Hivi ni vitisho, waache mara moja," Waziri wa Mambo ya Nje, Mheshimiwa Bernard Membe aliliambia Bunge. 

"Muda umefika wa kwenda kusaidia majirani zetu ili kuhakikisha  Wakongo wanaishi kwa amani na kufanya shughuli zao na hakuna wa kututisha na kuzuia majeshi yetu kwenda Kongo," alisema Waziri Membe.



Mwezi uliopita, kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo la M23, Bertrand Bisimwa, aliliandikia barua Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, akisema kuwa waasi hao wameshawahi kuyashinda majeshi "makubwa na yenye zana bora," akaonya kuwa hali hiyo itajirudia kwa wanajeshi wa Tanzania kama wakiendelea na "safari yao ya hatari."



Makundi kadhaa yenye silaha, ikiwemo M23, wanaendesha harakati zao za uasi mashariki mwa Kongo na wanapigania kuidhibiti nchi hiyo kubwa yenye maliasili za madini, kama vile dhahabu, urani, coltan, ambayo hutumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya elektroniki, ikiwemo simu za mkononi.

Waasi wa M23 waliuteka mji wa Goma Novemba 20, 2012 baada ya walinda amani kuondoka  katika mji huo wenye wakazi milioni moja. Wapiganaji wa M23 waliondoka katika mji huo Desemba 1,2013 baada ya makubaliano ya kusimamisha mapigano.

Waasi wa M23 walijiondoa katika jeshi la Kongo mwezi Aprili 2012 kupinga kile walichodai kuwa ni mwenendo mbaya ndani ya jeshi la Taifa (FARDC). Walikuwa wamejumuishwa katika jeshi chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2009.

Tangu mwezi Mei 2012, takriban watu milioni 3 wameyekimbia makazi yao katika eneo la mashariki mwa Kongo. Takriban watu milioni 2.5 ni wakimbizi wa ndani, huku zaidi ya watu 460,000 wamekimbilia katika nchi za Rwanda na Uganda.

Kongo imekuwa ikikabiliwa na matatizo matatizo kwa miongo kadhaa, kama vile umaskini uliokithiri, miondombinu mibovu, na vita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambavyo viliibuka tangu mwaka 1998 na kugharimu maisha ya zaidi ya watu milioni 5.5.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment