VIONGOZI WA UAMSHO WAFUTIWA KESI


MAHAKAMA ya Mwanakwerekwe, Zanzibar imefuta kesi iliyokuwa ikiwakabili viongozi kumi wa Jumuiya ya Uamsho, visiwani Zanzibar.

Mahakama hiyo, imefikia uwamuzi huo jana, wakati viongozi hao walipofikishwa Mahakamani hapo.
Kwa hivyo: Kutokana na hatua hio, viongozi hao sasa watakuwa wanakabiliwa na kesi inayoendelea katika mahakama kuu ya Vuga, mjini Zanzibar.

Mara ya mwisho viongozi hao wa Dini, walipofikishwa mahakama kuu, chini ya Jaji Fatma Hamid, kesi yao ilipangwa kusikilizwa tena Aprili 11, mwaka huu.

Jaji Fatma, aliuagiza upande wa mashtaka kupeleka mahakamani kwa maandishi, ombi la kuzuia kutolewa kwa dhamana kwa washtakiwa hao.
Jaji huyo aliongeza: Licha ya kwamba upande wa mashtaka umekata rufaa kuzuia kusikilizwa kwa ombi la dhamana, mahakama itaendelea kusikiliza kesi ya msingi pamoja na dhamana inayohusu viongozi hao.
Upande wa Mashtaka katika kesi hiyo unaongozwa Ramadhan Nassibu na Raya Msellem, huku upande wa utetezi unaongozwa na wakili, Salim Towfiq na wenzake..

CHANZO: MZALENDO.NET
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment