MLIPUKO WA BOMU WAITIKISA BENKI MAARUFU NCHINI SOMALIA

Dahabshiil bank in Mogadishu, Somalia (file photo)
Benki ya Dahabshiil mjini Mogadishu, nchini Somalia




Mlipuko wa bomu umeyatikisa makao makuu ya benki ya Dahabshiil mjini Mogadishu, nchini Somalia na kutatiza shughuliza benki hiyo inayoongoza kwa miamala ya kifedha nchini humo.

Bomu hilo lilipuka nje ya benki hiyo jana Jumanne, saa chache baada ya wapiganaji wa al-Shabab kuamuru kampuni hiyo kusimamisha shughuli zake katika maeneo wanayoyadhibiti.

Maafisa wa Polisi wanasema kuwa watu wawili walijeruhiwa katika mlipuko huo ulioisambaratisha milango ya ofisi na kulitapakaza eneo hilo kwa uchafu.

"Bomu la kuendeshwa kwa mtambo lilitegwa mbele ya benki ya Dahabshiil na makao makuu ya benki hiyo mjini Mogadishu na walinzi wawili wamejeruhiwa,” kapteni wa polisi Nur Hassan alisema.

Mapema, wapiganaji wa kundi la al-Shabab waliingia katika matawi ya benki ya  Dahabshiil katika maeneo wanayoyadhibiti na kutaka yafungwe, wakiituhumu kampuni hiyo kushirikiana na mashirika ambayo wameshayapiga marufuku katika maeneo yao.

Mashirika ya fedha kama Dahabshiil yameendelea kuwa na umuhimu mkubwa kwa uchumi wa Somalia ulioparaganyika, ambayo haina sekta imara ya kibenki baada ya miaka 20 ya mgogoro wa ndani ya nchi hiyo.

Serikali dhaifu ya nchi hiyo imekuwa ikipambana na wapiganaji wa al-Shabab kwa zaidi ya miaka 5 sasa, na kuungwa mkono na vikosi imara vya Umoja wa Afrika kutoka Uganda, Burundi, na Djibouti.

Somalia ambayo ipo katika eneo la Pembe ya Afrika, imeendelea kuwa miongoni mwa nchi zinazotoa idadi kubwa kabisa ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi duniani.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment